Andika Barua ( Microsoft Word)

Namna ya kuandika barua kwa kutumia Microfost Word(2003, 2007, 2010, 2013). Microsoft Word ni program mojawapo ya computer inayopatikana ndani ya Microsoft Office. Program hii hutumika kwenye computer zenye Windows Operating Systems  mfano: Windows XP, 7 , 8 , 10 .   Ili uipate Microsoft Word ni lazima uwe na Microsfot Office kwenye computer.

Kuangalia kama Microsoft Word ipo, fata njia mojawapo.

  • Bonyeza Start au Windows kwenye keyboard yako, chagua All Programs -> Microsoft Office -> Microsoft Word
  • Au, Bonyeza Start halafu search Word na uchague Microsoft Word

Usipoiona katika njia hizo , tafadhari install Microsoft Office kwenye computer yako kwanza au wasiliana nasi kwa msaada.

Iwapo umefanikiwa kufungua Microsoft Word na program imefunguka mpaka umeona ukurasa mweupe, iwapo haifika kwenye karatasi nyeupe chagua new blank document na itaenda kwenye karatasi nyeupe.

Hongera: Umefanikiwa kufungua mpaka sehemu ya kuandika. Kabla haujaanza kuandika tafadhari bonyeza File->Save itakuuliza sehemu unapotaka kuisave barua yako hakikisha unachagua sehemu ambayo unaweza kuikumbuka ilipo barua yako baada ya kumaliza kuandika. Ukiiacha ichague itasave barua yako kwenye Documents au My Documents folder.

office

Anza Kuandika: Ndiyo andika barua yako unavyotaka iwe hakikisha unabonyeza File->Save ili iwe inajisave au shortcut ni kubonyeza Ctrl+S na ukimaliza kutype hakikisha unabonyeza File->Save.

Tafadhari tembelea blog yetu mara kwa mara kufahamu zaidi na zaidi kuhusiana na program hii na mafunzo mengine mengi.