Namna ya kuconnect modem kwenye Ubuntu/Linux

Kwa watumiaje wa Linux Operating System haswaa Ubuntu au Linux Mint kumwekuwa na mswali mengi ya namna wanayoweza kuconnect modem zao wanapokuwa ndiyo wamemaliza kuinstall au wanapojaribu kuziweka kwa mara ya kwanza.

Usihofu fuata njia hizi:-

ubuntumodem

menu_018

  • Chomeka modem yako ikiwa na line ya simu ndani.
  • Nenda sehemu yenye alama ya mnara kwenye taskbar yako bonyeza hapo.
  • Chagua Enable Networking ( Kama imeshachaguliwa endelea chini).
  • Chagua Edit Connection – > Add
  • Chagua Mobile Broadband -> Create
  • Chagua Any Device ->Next
  • Chagua Nchi->Next
  • Chagua Mtandao Wako->Next
  • Chagua Plan weka Default->Next
  • Chagua Apply

 

 

Sasa mtandao wako utakuwa tayari kuconnect na internet, nenda kwenye mnara na uchague mtandao wako na itaconnect yenyewe.Usipoona mtandao wako hakikisha kitufe cha Enable Networking na Enable Mobile Broadband vina alama ya vema() pembeni yake.