Namna ya kushare link kwenye internet

Umekuwa ukijiuliza watu wanawezaje kushare kushare vitu kutoka katika site fulani kwenda site fulani. Mfano: Kutoka Youtube kwenda Facebook . Jibu ni hili

Site nyingi zinaruhusu sharing ya content zao directly kutoka katika site kwa kutumia Sharing Button kama hii ya kwenye picha.

sharingyoutube

Lakini pale unapotaka kushare page ambayo haina sharing button je ni kipi unafanya, mfano instagram profile ya mtu, blog nk.

Katika kila kurasa ya tovuti juu yake kuna kuwa na anwani ya kurasa, Ndiyo anwani na huwa hafanani baina ya kurasa moja na nyingine. Anwani hii ni yale maandishi Mfano: https://www.google.com/#q=anwani+hii Hii husimama kuonesha kurasa uliyopo.

Sasa ukihitaji kushare kurasa hiyo unachotakiwa kufanya ni:-

linkefacebook

  • Nenda sehemu ya anwani
  • Bonyeza hiyo anwani
  • Ikiwa yote itakuwa na rangi nyingi baada ya kubonyeza hiyo anwani ruka mstari mstari huu endelea na mwingine. Ikiwa umebonyeza na haijabadilika rangi tumia mouse yako kuipitisha ukiwa umeikandamiza kutokea kushoto kwenda kulia mpaka maneno yote yabadilike rangi . Njia rahisi ni kuponyeza Ctrl+A kama unatumia computer hii tunaita Ku-highlight maneno.
  • Sasa bonyeza mouse upande wa kulia na uchague copy, au bonyeza Crtl+C kwenye computer yako.
  • Safi, sasa nenda sehemu unapotaka kuiweka au kuishare hiyo page na u-paste hapo au bonyeza Ctrl+V kwenye computer yako.

Ahsante, kwa kutembelea ukurasa wetu tafadhari tusaidie kwa kushare na kualika wengine pia waje kujifunza nasi.

Advertisements