Wezesha simu yako na huduma za internet (Android)

Kuunganisha simu yako na huduma za internet kwa watumiaji wa Android. Njia hii na yakuunganisha kwa mtumiaji husika mwenyewe(manually) kuna njia nyingine iliyorahisi pale unapoweka tu line(sim card) yako kwenye simu huwa unatumiwa settings za internet na mtumiaji unatakiwa kuzisave.

Iwapo hauna setting za internet kwenye simu yako fata maelekezo yafuatayo. Hii ni watumiaji wa Airtel, Tigo , Vodacom , Zantel na Halotel.

 • Washa simu yako hakikisha una kifurushi cha internet vinginevyo ukiwasha internet gharama za kawaida zitatozwa.
 • Nenda Mipangilio(Settings).
 • Tafuta Wireless & Networks na Bonyeza More.
 • Chagua Mobile Networks.
 • Chagua Access Point Names.
 • Bonyeza vidoti vitatu au Menu wakati mwingine alama ya + au bonyeza Add New.
 • Chagua New APN.
 • Nenda kwenye name na uandike jina la kampuni kama nilivyoorodhesha hapa chini
  • Zantel andika ZANTEL.
  • Vodacom andika Vodacom Internet.
  • Airtel andika AIrtel Internet.
  • Halotel andika HALOTEL_APN.
 • Kicha nenda kwenye APN na undike kama ifuatavyo
  • Kwa watumiaji wa Airtel, Vodacom na Halotel wataandika internet.
  • Kama unatumia Zantel utaandika znet.
 • Save hizo settings.
 • Sasa nenda kwenye settings->Mobile Networks->Access Point Names-> Na uchague Setting uliyosave iwe On.
 • Washa Mobile Data ( Setting->Mobile Networks->Data enabled).

Hongera umefanikiwa kuiwezesha simu yako na huduma za internet.