Tengeneza akaunti yako ya Barua Pepe (Gmail)

Namna ya kutengeneza akaunti ya barua pepe. Zoezi hili linafanyika kwenye computer iliyounganishwa na internet.

    1. Fungua browser(Mozilla Firefox, Internet Explorer nk) yako.
    2. Nenda http://www.google.com

       google

    3. Chagua Gmail upande wako wa kulia
    4. Chagua Create an account
    5. Jaza fomu itakayotokea. Wakati wa kujaza hakikisha.

         22

     1. Username ndiyo itakuwa jina la email yako, hazifanani iwapo itakataa jua username hiyo imeshachukuliwa itabidi uandike nyingine.
     2. Utaandika neno la siri(password) na chini yake utalirudia(confirm password). Angalizo lazima neno la siri na anwani ya barua pepe uvikumbuke.
     3. Namba ya simu ni muhimu ukaweka , itakusaidia ukisahau neno siri.
     4. Your Current Email ( Sio Lazima unaweza kuacha). Kama unayo email nyingine unaweza kuindika hapa.
    6. Bonyeza Next Step
    7. Kubali mkataba wako na Gmail kwa kuchagua I Agree / I accept
    8. Chagua Continue to gmail
    9. Hongera!!!! Tumeshatengeneza email sasa tunaweza kuitumia

33

 

Kumbuka: Usije kusahau anwani ya barua pepe yako na neno la siri.