Activate Windows yako kwa kutumia Command

Kuactivate Windows yako kwa kutumia command hii haitakufanya upate uhakika wa kudumu hili litakupatia siku 30 zaidi huku ukijipanga kununua Windows yako kutoka kwa mawakala. Hii inafanya kazi kwenye Windows Xp/7/8 na 10.

Angalizo: Trick hii ni ya kuactivate kwa muda wa siku 30 tu, Swahiliware inashauri kununua Windows orijino ili kuweza kupata ufanisi zaidi wa Windows yako.

Mfano Windows yako inaonesha maandishi kama haya pembeni

1

Yanayosema, This copy of Windows is not Genuine. Na kuonesha rangi nyeusi tu nyuma hata ukibadilisha picha. Fuata hatua zifuatazo.

  • Bonyeza Start na andika cmd
  • Chagua cmd kwa kubonyeza mouse ya kulia(right click).
  • Chagua Run as administrator

2

  • Andika maneno haya kama yalivyo slmgr /rearm

3

  • Subiri mpaka hiko kiboksi kitokee, chagua OK.
  • Zima halafu washa computer yako.

Hongera tumefanikiwa kuactivate Windows kwa muda.